DSpace Repository

Tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya shahada ya umahiri wa elimu katika kiswahili na elimu ya chuo kikuu cha Rwanda ndaki ya elimu

Show simple item record

dc.contributor.author Nsengimana, Leon
dc.date.accessioned 2026-01-21T14:34:54Z
dc.date.available 2026-01-21T14:34:54Z
dc.date.issued 2023-10
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2842
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Utafiti huu ulilenga kutathimini nafasi ya ufundishaji na ujifunzaji katika uimarishaji wa Kiswahili kama lugha rasmi nchini Rwanda. Hii inatokana na Kiswahili kufanywa kuwa lugha rasmi nchini Rwanda tangu mwaka 2017 Kwa hiyo, kwanza, utafiti huu ulikuwa na malengo mawili: Kwanza, kubainisha nafasi ya ufundishaji na ujifunzaji katika uimarishaji wa Kiswahili kama lugha rasmi nchini Rwanda. Pili, kujadili vikwazo vinavyokabili ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha rasmi nchini Rwanda pamoja na kupendekeza suluhu. Nadharia ya Mwingiliano wa Kijamii ndiyo iliyoongoza utafiti huu ambao ulikuwa wa kitaamuli. Walengwa wa utafiti husika walikuwa wanafunzi wa madarasa ya Kiswahili, walimu wa Kiswahili, wakurugenzi na viongozi wa Kiswahili katika taasisi tofauti nchini Rwanda. Sampuli ya wanafunzi 30, walimu 3, wakurugenzi 3 na viongozi wa Kiswahili 3 ilipatikana kwa kutumia usampulishaji lengwa. Ukusanyaji wa data ulitumia mbinu mbili ambazo ni usaili na uchanganuzi matini. Data za kitaamuli zilizokusanywa, ziliwasilishwa na kuchanganuliwa kwa kutumia madondoo na maelezo. Aidha, Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa ufundishaji na ujifunzaji una mchango mkubwa katika uimarishaji wa Kiswahili kama lugha rasmi nchini Rwanda. Hii ni kwa sababu ufundishaji na ujifunzaji unakuza siyo tu stadi, msamiati na ufahamu wa sheria za sarufi ya Kiswahili bali pia unatoa mahali mwafaka pa kuzungumzia lugha ya Kiswahili. Vilevile, matokeo ya utafiti yameonesha kwamba kuna vikwazo kadhaa vinavyokabili walimu wanapofundisha Kiswahili katika shule za sekondari nchini Rwanda. Vikwazo hivyo ni pamoja na mwingiliano wa lugha, ukosefu wa vifaa vya kuelimishia na kusomea Kiswahili, uhaba wa walimu wenye ujuzi na uwezo wa kufundisha Kiswahili na mtazamo hasi wa wanafunzi kuhusu lugha ya Kiswahili. Isitoshe, baada ya kudhihirisha vikwazo, utafiti ulioibua tasinifu hii umependekeza suluhu za vikwazo vinavyokabili walimu wanapofundisha Kiswahili katika shule za sekondari nchini Rwanda. Suluhu hizo ni pamoja na matumizi ya mazoezi mengi ya mazungumzo, utumiaji wa vifaa vya kiteknolojia, kuimarisha na kuendeleza mafunzo kwa walimu wa Kiswahili na kuondoa mtazamo hasi kuhusu Kiswahili. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Shahada ya umahiri wa elimu katika kiswahili en_US
dc.subject Elimu ya chuo kikuu cha Rwanda ndaki ya elimu en_US
dc.subject Kiswahili en_US
dc.title Tasinifu iliyowasilishwa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya shahada ya umahiri wa elimu katika kiswahili na elimu ya chuo kikuu cha Rwanda ndaki ya elimu en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account