DSpace Repository

Ukuzaji wa tafakuri bunifu kupitia ufundishaji wa fasihi kwa wanafunzi wa kiswahili shule teule za sekondari wilayani Kicukiro

Show simple item record

dc.contributor.author Niyirora Emmanuel
dc.date.accessioned 2026-04-14T17:01:20Z
dc.date.available 2026-04-14T17:01:20Z
dc.date.issued 2022-06
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2746
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Tasnifu hii imetokana na utafiti uliokusudia kuchunguza Ukuzaji wa Tafakuri Bunifu Kupitia Ufundishaji wa Fasihi kwa Wanafunzi wa Kiswahili, Shule Teule za Sekondari Wilayani Kicukiro. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi mawili: kubainisha nafasi ya fasihi andishi ya Kiswahili katika ukuzaji wa tafakuri bunifu miongoni mwa wanafunzi katika shule za sekondari nchini Rwanda, na pia kuunda mwongozo wa ufundishaji wa tafakuri bunifu kupitia fasihi miongoni mwa wanafunzi katika shule za sekondari nchini Rwanda. Ili kukamilisha malengo haya mahususi, data za msingi na data za upili zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji, uchanganuzi matini na usaili. Wango la utafiti huu lilikuwa walimu wa Kiswahili na wakuu wa masomo walioteuliwa katika shule za sekondari Wilayani Kicukiro. Sampuli ya utafiti ilipatikana kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Aidha, utafiti ulitumia mkabala wa kitaamuli. Uchanganuzi na ufasiri wa data uliegemezwa kwenye Nadharia ya Utambuzi. Licha ya matokeo ya utafiti kuonesha kuwa fasihi ina nafasi muhimu katika ufundishaji wa tafakuri bunifu, ilionekana kuwa baadhi ya walimu hawafanikiwi kujumuisha stadi ya tafakuri bunifu sio tu katika maandalio ya masomo, bali pia katika ufundishaji na tathmini. Hii inatokana na sababu zifuatazo: Walimu kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu ufundishaji wa stadi za tafakuri bunifu na utekelezaji wa MUU, muda mfupi wa kuandaa kazi za ufundishaji na majukumu mengi ambayo walimu wanapaswa kutimiza. Ili kukabiliana na vikwazo hivyo, matokeo ya utafiti yamebainisha mwongozo unaopaswa kufuatwa na walimu katika ufundishaji wa stadi za tafakuri bunifu kupitia fasihi. Mwongozo huu unaweka mkazo katika utumizi wa: kazi za makundi, kazi za uigizaji, kazi za fikiri-jozi-changia na midahalo. Aidha, matokeo ya utafiti yamebainisha mikakati tofauti inayoweza kutumiwa na walimu wa fasihi ili kuimarisha stadi za tafakuri bunifu miongoni mwa wanafunzi. Mikakati hiyo ni pamoja na utumiaji wa michezo ya maneno, maswali bunifu, kazi wazi, hadithi duara na matumizi ya maswali ya mafumbo. Mwisho, tasnifu hii imedhihirisha mfano wa namna ya kufundisha fasihi kwa kuegemea katika mwongozo wa utumizi wa fasihi katika kukuza tafakuri bunifu. Aidha, tasnifu hii inapendekeza kwamba wadau wote wa sekta ya elimu wanalazimika kuungana mkono ili kuimarisha ufundishaji wa stadi za tafakuri bunifu na stadi nyingine za karne ya ishirini na moja miongoni mwa wanafunzi. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Kiswahili en_US
dc.title Ukuzaji wa tafakuri bunifu kupitia ufundishaji wa fasihi kwa wanafunzi wa kiswahili shule teule za sekondari wilayani Kicukiro en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account