University of Rwanda Digital Repository

Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa kiswahili katika shule za ufundi nchini Rwanda: mfano wa shule za ufundi wilayani Karongi

Show simple item record

dc.contributor.author Bucyedusenge, Vincent
dc.date.accessioned 2025-08-27T12:25:21Z
dc.date.available 2025-08-27T12:25:21Z
dc.date.issued 2023-10
dc.identifier.uri http://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2315
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Utafiti husika wenye anwani, “Changamoto za Ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule za Ufundi Nchini Rwanda: Mfano wa Shule za Ufundi Wilayani Karongi” ulilenga kutimiza malengo mahususi mawili ambayo ni kuchunguza changamoto ambazo zinakabili ufundishaji na ujifunzaji wa lugha wa Kiswahili na pia kupendekeza mikakati ya kukabili changamoto ambazo zinakabili ujifunzaji na ufundishaji wa Kiswahili kwa wajifunzaji wa shule sekondari za ufundi wilayani Karongi. Ili kukamilisha malengo haya, data za msingi na data za upili zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji, uchanganuzi matini na usaili. Wango la utafiti huu lilikuwa wanafunzi wa madarasa ya Kiswahili, walimu wa Kiswahili na viongozi wa masomo wa shule za sekondari za ufundi kwenye Wilaya ya Karongi. Sampuli ya utafiti ilipatikana kwa kutumia mbinu ya sampuli lengwa. Utafiti wetu ulitumia mkabala wa kitaamuli. Uchanganuzi na ufasiri wa data uliegemezwa kwenye Nadharia ya Utabia. Licha ya tafiti kadhaa kuonesha kuwa Kiswahili ni lugha muhimu, matokeo ya utafiti wetu yameonesha kwamba kuna changamoto ambazo zinakabili ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kwenye shule za sekondari za ufundi kwenye Wilaya ya Karongi. Hii inatokana na ukosefu wa walimu wenye uwezo, ukosefu wa vifaa na zana za kufundishia Kiswahili, muda usiotosheleza ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili na ukosefu wa msukumo binafsi wa kujifunza Kiswahili miongoni mwa wanafunzi. Ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na changamoto hizo, matokeo ya utafiti yamebainisha mambo yanayoweza kushiriki katika uimarishaji wa ujifunzaji pamoja na ufundishaji wa lugha ya Kiswahili. Mambo hayo yanasisistizia maandalizi ya mafunzo na warsha kwa walimu wa Kiswahili, utumiaji wa vifaa vya TEHAMA, utengenezaji na ufaraguzi wa zana za kufundishia Kiswahili na ukuzaji wa motisha ya kujifunza Kiswahili miongoni mwa wanafunzi. Aidha, matokeo ya utafiti yamebainisha mikakati ya kukabili changamoto ambazo zinakabili walimu wanapofundisha lugha ya Kiswahili. Mikakati hiyo ni pamoja na: utumiaji wa mbinu ya ujifunzaji wa lugha kwa ushirikiano, utumiaji wa mbinu ya ujifunzaji lugha kijumuia na utumiaji wa mbinu ya ujifunzaji wa lugha unoegemea katika uwezo. Mwisho, utafiti huu umependekeza kuwa watu wanaohusika katika elimu kwenye nchi ya Rwanda, wanalazimika kuungana mkono ili kuitia jeki ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwenye shule za sekondari za ufundi nchini Rwanda. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Ufundishaji wa Kiswahili en_US
dc.subject ujifunzaji wa Kiswahili en_US
dc.title Changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa kiswahili katika shule za ufundi nchini Rwanda: mfano wa shule za ufundi wilayani Karongi en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Repository


Browse

My Account