DSpace Repository

Nafasi ya fasihi andishi katika ukuzaji wa stadi za mawasiliano: mfano wa shule za sekondari teule wilayani Nyanza

Show simple item record

dc.contributor.author Idahemuka, Magnifique
dc.date.accessioned 2026-05-07T12:30:49Z
dc.date.available 2026-05-07T12:30:49Z
dc.date.issued 2024-09
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2873
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Tasnifu hii inajadili nafasi ya fasihi andishi katika ukuzaji wa stadi za mawasiliano: mfano wa shule za sekondari teule wilayani Nyanza. Utafiti uliofanyika ulikusudia kutimiza malengo mahususi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa kutathmini nafasi ya fasihi andishi katika ukuzaji wa stadi za mawasiliano katika shule za sekondari sekondari teule wilayani Nyanza. Lengo la pili lilikuwa kuunda miongozo ya kutumia fasihi andishi katika ukuzaji wa stadi za mawasiliano katika shule za sekondari teule wilayani Nyanza. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mawasiliano. Aidha, katika ukusanyaji wa data, utafiti ulitumia usaili, ushuhudiaji na uchanganuzi matini. Wango la utafiti lilihusisha walimu wa Kiswahili na wanafunzi wanaojifunza katika mchepuo wa LFK. Mbinu ya usampulishaji lengwa ilitumiwa ili kupata sampuli ya walimu 9 na wanafunzi 93. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba fasihi andishi ina nafasi kubwa katika ukuzaji wa stadi za mawasiliano katika lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari teule wilayani Nyanza. Kwanza, fasihi inakuza uwezo wa kuwasiliana. Pili, inakuza stadi za lugha kama kusoma, kuandika, kusikiliza na kuzungumza. Tatu, inakuza stadi ya ujasiri. Nne, fasihi andishi inachangia katika kukuza utambuzi wa hisia kwa wanafunzi. Hata hivyo, kwenye shule za sekondari teule wilayani Nyanza, walimu wa Kiswahili wanakumbana na changamoto kama mtazamo finyu kuhusu stadi za mawasiliano na tathmini zinazosisitiza zaidi stadi za kuandika na kusoma. Vilevile, kwenye shule teule kuna changamoto ya muda usiotosha na mbinu za ufundishaji zisizofaa ambazo hutumiwa na walimu kwa kukuza stadi za mawasiliano kupitia ufundishaji wa stadi za mawasiliano katika Kiswahili. Zaidi ya hayo, utafiti umeunda miongozo ya kutumia fasihi andishi kukuza stadi za mawasiliano katika shule za sekondari teule wilayani Nyanza. Miongozo hii inajikita katika utumiaji wa mbinu ya mawasiliano ya mtu mmoja kwa mwingine, uumbaji wa mazingira salama ya kujifunzia na uhusiano wenye msaada na usikilizaji kwa makini. Isitoshe, utafiti uliofanyika umedhihirisha mfano wa namna ya kufundisha fasihi kwa kuegemea kwenye miongozo ya utumizi wa fasihi andishi katika kukuza stadi za mawasiliano miongoni mwa wanafunzi. Mwisho, utafiti umependekeza kwamba walimu wa fasihi andishi wanalazimika kufanya juu chini ili kutumia mbinu za ufundishaji mabazo zinakuza stadi za mawasiliano katika lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu mawasiliano fasha katika lugha hii yanaweza kuwaletea wanafunzi manufaa tele. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Stadi za mawasiliano en_US
dc.title Nafasi ya fasihi andishi katika ukuzaji wa stadi za mawasiliano: mfano wa shule za sekondari teule wilayani Nyanza en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account