DSpace Repository

Mchango wa tehama katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi ya kuzungumza katika lugha ya kiswahili: mfano wa shule teule za sekondari Nyamasheke-Rwanda

Show simple item record

dc.contributor.author Niyobuhungiro, Emmanuel
dc.date.accessioned 2026-05-11T13:50:13Z
dc.date.available 2026-05-11T13:50:13Z
dc.date.issued 2024-10
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2874
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Utafiti uliofanyika ulikuwa na lengo la jumla la kuchunguza mchango wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi ya kuzungumza katika lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari teule wilayani Nyamasheke nchini Rwanda. Malengo mahususi ya utafiti yalikuwa mawili. Kwanza, kubainisha nafasi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi ya kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari teule wilayani Nyamasheke nchini Rwanda. Pili, kuunda miongozo ya utumiaji wa TEHAMA katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa stadi ya kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari teule wilayani Nyamasheke nchini Rwanda. Kwa kutimiza malengo haya, utafiti uliegemezwa katika Nadharia ya Kuunganishwa. Wango la utafiti lilihusisha wakurugenzi, wakuu wa masomo, wanafunzi na walimu katika shule za sekondari teule wilayani Nyamasheke. Sampuli ya utafiti ilihusisha wanafunzi 115 wa kidato cha sita. Wanafunzi hawa waliteuliwa kwa makusudi kwa kuwa ndio ambao wana umahiri katika Kiswahili ukilinganisha na wanafunzi wa vidato vya chini. Aidha, sampuli ilihusisha walimu 5, wakurugenzi 5 na wakuu wa masomo 5 ambao waliteuliwa kwa kutumia usambulishaji lengwa. Ili kukusanya data, mbinu za usaili, uchambuzi matini na ushuhudiaji zilitumiwa. Aidha, matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba TEHAMA ina nafasi kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kuzungumza Kiswahili. Kwanza, TEHAMA hurahisisha ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kuzungumza. Pili, TEHAMA inawezesha walimu na wanafunzi wa lugha kupata zana za kisasa za kufundishia stadi za kuzungumza. Tatu, TEHAMA ina nafasi katika kuongeza hamasa ya kuzungumza Kiswahili miongoni mwa wanafunzi. Nne, TEHAMA inatumiwa ili kuwezesha wanafunzi kuwasiliana na wazawa wa Kiswahili kwa urahisi. Hata hivyo, matokeo yanaonesha changamoto katika matumizi ya TEHAMA, ikiwa ni pamoja na uhaba wa zana za TEHAMA na ukosefu wa ujuzi wa kutumia programu za TEHAMA. Ili kuepukana na changamoto hizi, tunapendekeza kuandaa semina kwa walimu wa Kiswahili, kupanga ratiba ya matumizi ya chumba cha kompyuta, kuongeza zana za TEHAMA kwa ajili ya kufundisha stadi za kuzungumza Kiswahili. Mwisho, utafiti umetoa miongozo ya utumiaji wa michezo ya KiTEHAMA na mikutano ya video mtandaoni na utumiaji wa programu za mtandaoni za kufundishia na kujifunzia stadi za kuzungumza Kiswahili. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Tehama en_US
dc.subject , Ufundishaji na Ujifunzaji en_US
dc.subject Stadi ya Kuzungumza en_US
dc.title Mchango wa tehama katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi ya kuzungumza katika lugha ya kiswahili: mfano wa shule teule za sekondari Nyamasheke-Rwanda en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account