DSpace Repository

Athari za kifonolojia za Kinyarwanda katika ujifunzaji wa Kiswahili: mfano wa shule za sekondari teule wilayani Bugesera, Rwanda

Show simple item record

dc.contributor.author Bigirimana, Jean de Dieu
dc.date.accessioned 2026-05-14T08:32:30Z
dc.date.available 2026-05-14T08:32:30Z
dc.date.issued 2024-10
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2881
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Utafiti wetu ulilenga kuchunguza athari za kifonolojia za Kinyarwanda katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo, malengo mahususi ya utafiti yalikuwa mawili. Mosi, kubainisha athari za kifonolojia za lugha ya Kinyarwanda katika ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari teule wilayani Bugesera, Rwanda. Pili, kubainisha mikakati ya kukabili athari za kifonolojia za Kinyarwanda katika ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari teule wilayani Bugesera. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Linganuzi. Wango la utafiti lilikuwa walimu wa Kiswahili na wanafunzi wa shule za sekondari teule wilayani Bugesera. Sampuli ya utafiti ilikuwa walimu wa Kiswahili 7 na wanafunzi 76 ambao walichaguliwa kwa kutumia usampulishaji lengwa. Mbinu za uchambuzi matini, ushuhudiaji na mahojiano zilitumika kukusanya data za kitaamuli ambazo zilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa madondoo na maelezo. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, kuna athari za kifonolojia katika ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za sekondari teule wilayani Bugesera. Athari hizo ni pamoja na uchopekaji, udondoshaji, ubadilishaji wa fonimu na mpangilio mbaya wa mofimu katika maneno. Vilevile, matokeo yamebainisha sababu za athari hizo. Sababu ya kwanza ni ukosefu wa mafunzo ya kina ya fonetiki na fonolojia kwa wanafunzi. Pili, ni mazingira ya nyumbani na shuleni ambapo Kinyarwanda kinatumika zaidi kuliko Kiswahili.Tatu, ni shule kutilia mkazo zaidi ufundishaji wa sarufi na fasihi kuliko fonolojia. Isitoshe, matokeo ya utafiti yamebainisha mikakati ya kukabili athari hizo. Mikakati iliyotolewa ni pamoja na kulinganisha fonolojia ya Kinyarwanda na ya Kiswahili, kutoa mazoezi ya kutosha yanayohusiana na fonolojia ya Kiswahili na kuanzisha klabu za Kiswahili katika shule. Kwa hivyo, utafiti ulipendekeza ushirikiano baina ya wanafunzi, walimu na viongozi wa shule ili kuondoa athari za kifonolojia za Kinyarwanda katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Fonolojia en_US
dc.subject Athari za Kifonolojia na Ujifunzaji wa Kiswahili en_US
dc.title Athari za kifonolojia za Kinyarwanda katika ujifunzaji wa Kiswahili: mfano wa shule za sekondari teule wilayani Bugesera, Rwanda en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account