Abstract:
Utafiti uliofanyika ulilenga kuchunguza mchango wa TEHAMA katika ufundishaji wa
fasihi andishi katika shule za sekondari wilayani Nyagatare nchini Rwanda. Uchunguzi
huu ulifanyika kwa kutimiza malengo mahususi mawili. Kwanza, kubainisha mchango
wa TEHAMA katika ufundishaji wa fasihi andishi katika shule za sekondari teule
wilayani Nyagatare nchini Rwanda. Pili, kuunda miongozo ya utumiaji wa TEHAMA ili
kuleta ufanisi wa ufundishaji wa fasihi katika shule za sekondari wilayani Nyagatare
nchini Rwanda. Ili kutimiza malengo haya, utafiti uliongozwa na Nadharia ya
Uunganisho. Mbinu ya usaili, ushuhudiaji na uchanganuzi matini zilitumiwa ili
kukusanya data. Wango la utafiti lilikuwa, viongozi wa shule, wakuu wa masomo,
walimu wa Kiswahili na wanafunzi wa mchepuo wa LFK. Sampuli ya utafiti ilihusisha
wanafunzi 103, walimu wa Kiswahili kumi, wakuu wa masomo watano na wakurugenzi
watano ambao waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Data za utafiti
zilichanganuliwa, kufasiliwa na kuwasilishwa kwa kutumia njia ya madondoo na
maelezo. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba TEHAMA ina mchango mkubwa
katika ufundishaji wa fasihi andishi katika shule za sekondari teule wilayani Nyagatare
kwa sababu zifuatazo: Kwanza, TEHAMA inaleta urahisi katika upatikanaji wa nyenzo
za ufundishaji na ujifunzaji kama vitabu vya kielektroniki na video za ufafanuzi. Pili,
TEHAMA inawezesha wanafunzi kujifunza fasihi andishi ya Kiswahili kwa
kuwaunganisha na wanafunzi wengine duniani kote kupitia mitandao ya kijamii na tovuti
tofauti. Tatu, TEHAMA inawezesha wanafunzi kujifunza stadi mpya zinazohitajika
katika fasihi andishi kama vile stadi ya ubunifu na kutafakari kitunduizi. Nne, TEHAMA
inawapa wanafunzi motisha ya kujifunza fasihi andishi ya Kiswahili. Mwisho, matokeo
ya utafiti yameonesha kwamba matumizi ya TEHAMA yanarahisisha ufundishaji wa
fasihi andishi ya Kiswahili kwa sababu wanafunzi huvutiwa zaidi kwa kutumia vifaa vya
kidijiti kama vile simu na kompyuta. Zaidi ya hayo, matokeo ya utafiti yamebainisha
changamoto za ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili kupitia TEHAMA katika shule
za sekondari teule wilayani Nyagatare. Changamoto hizo ni ukosefu wa zana za
kufundishia na mbinu za ufundishaji zinazotumiwa na walimu. Isitoshe, matokeo ya
utafiti yametoa miongozo ya utatuaji wa zana za kufundishia fasihi andishi ya Kiswahili
kupitia TEHAMA katika shule za sekondari wilayani Nyagatare nchini Rwanda.
Miongozo hii unahusisha utumiaji wa projekta na slaidi, usimulizi wa kidijiti na mitandao
ya kijamii. Mwisho, ili kukabiliana na changamoto za ufundishaji wa fasihi andishi ya
Kiswahili kupitia TEHAMA, matokeo ya utafiti yamependekeza mbinu tofauti za
ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili na kutilia mkazo kwenye maandalizi y