DSpace Repository

Mchango wa tehama katika ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili katika shule za sekondari teule wilayani Nyagatare nchini Rwanda

Show simple item record

dc.contributor.author Tulinumukiza, Froduard
dc.date.accessioned 2026-05-14T09:39:58Z
dc.date.available 2026-05-14T09:39:58Z
dc.date.issued 2024-10
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2891
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Utafiti uliofanyika ulilenga kuchunguza mchango wa TEHAMA katika ufundishaji wa fasihi andishi katika shule za sekondari wilayani Nyagatare nchini Rwanda. Uchunguzi huu ulifanyika kwa kutimiza malengo mahususi mawili. Kwanza, kubainisha mchango wa TEHAMA katika ufundishaji wa fasihi andishi katika shule za sekondari teule wilayani Nyagatare nchini Rwanda. Pili, kuunda miongozo ya utumiaji wa TEHAMA ili kuleta ufanisi wa ufundishaji wa fasihi katika shule za sekondari wilayani Nyagatare nchini Rwanda. Ili kutimiza malengo haya, utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uunganisho. Mbinu ya usaili, ushuhudiaji na uchanganuzi matini zilitumiwa ili kukusanya data. Wango la utafiti lilikuwa, viongozi wa shule, wakuu wa masomo, walimu wa Kiswahili na wanafunzi wa mchepuo wa LFK. Sampuli ya utafiti ilihusisha wanafunzi 103, walimu wa Kiswahili kumi, wakuu wa masomo watano na wakurugenzi watano ambao waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Data za utafiti zilichanganuliwa, kufasiliwa na kuwasilishwa kwa kutumia njia ya madondoo na maelezo. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba TEHAMA ina mchango mkubwa katika ufundishaji wa fasihi andishi katika shule za sekondari teule wilayani Nyagatare kwa sababu zifuatazo: Kwanza, TEHAMA inaleta urahisi katika upatikanaji wa nyenzo za ufundishaji na ujifunzaji kama vitabu vya kielektroniki na video za ufafanuzi. Pili, TEHAMA inawezesha wanafunzi kujifunza fasihi andishi ya Kiswahili kwa kuwaunganisha na wanafunzi wengine duniani kote kupitia mitandao ya kijamii na tovuti tofauti. Tatu, TEHAMA inawezesha wanafunzi kujifunza stadi mpya zinazohitajika katika fasihi andishi kama vile stadi ya ubunifu na kutafakari kitunduizi. Nne, TEHAMA inawapa wanafunzi motisha ya kujifunza fasihi andishi ya Kiswahili. Mwisho, matokeo ya utafiti yameonesha kwamba matumizi ya TEHAMA yanarahisisha ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili kwa sababu wanafunzi huvutiwa zaidi kwa kutumia vifaa vya kidijiti kama vile simu na kompyuta. Zaidi ya hayo, matokeo ya utafiti yamebainisha changamoto za ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili kupitia TEHAMA katika shule za sekondari teule wilayani Nyagatare. Changamoto hizo ni ukosefu wa zana za kufundishia na mbinu za ufundishaji zinazotumiwa na walimu. Isitoshe, matokeo ya utafiti yametoa miongozo ya utatuaji wa zana za kufundishia fasihi andishi ya Kiswahili kupitia TEHAMA katika shule za sekondari wilayani Nyagatare nchini Rwanda. Miongozo hii unahusisha utumiaji wa projekta na slaidi, usimulizi wa kidijiti na mitandao ya kijamii. Mwisho, ili kukabiliana na changamoto za ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili kupitia TEHAMA, matokeo ya utafiti yamependekeza mbinu tofauti za ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili na kutilia mkazo kwenye maandalizi y en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Tehama en_US
dc.subject Andishi ya Kiswahili en_US
dc.subject Fasihi andishi en_US
dc.title Mchango wa tehama katika ufundishaji wa fasihi andishi ya Kiswahili katika shule za sekondari teule wilayani Nyagatare nchini Rwanda en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account