DSpace Repository

Uchunguzi wa makosa ya kimatamshi na kiotografia yanayofanywa na wanafunzi wa kiswahili: Mfano wa shule teule za sekondari wilayani Nyarugenge, Rwanda

Show simple item record

dc.contributor.author Sebazungu, Pascal
dc.date.accessioned 2026-01-19T17:31:53Z
dc.date.available 2026-01-19T17:31:53Z
dc.date.issued 2025-10
dc.identifier.uri https://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2824
dc.description Tasnifu ya Uzamili / Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Utafiti huu ulichunguza makosa ya kimatamshi na kiotografia yanayofanywa na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za sekondari Wilayani Nyarugenge, Rwanda. Malengo mahsusi ya utafiti yalikuwa kubainisha makosa ya kimatamshi na kiotografia yanayofanywa wa wanafunzi wa Kiswahili wa kidato cha tano, kufafanua sababu zinazosababisha makosa ya kimatamshi na kiotografia yanayofanywa na wanafunzi wa Kiswahili wa kidato cha tano, na kubainisha mikakati ya kutumiwa na walimu wa Kiswahili kukabili makosa ya kimatamshi na kiotografia miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha tano. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano, ushuhudiaji, na udurusu wa nyaraka kutoka shule teule za sekondari za Wilaya ya Nyarugenge ambazo ni Shule ya Sekondari ya Camp Kigali, GS Cyahafi, na Kigali Leading TVT School. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Makosa iliyoasisiwa na Corder (1967). Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa wanafunzi hufanya makosa ya kimatamshi na kiotografia katika kazi mbalimbali za kimazungumzo na kimaandishi. Makosa haya yanajumuisha athari za Kinyarwanda katika matamshi ya sauti za Kiswahili kama vile /b/, /dh/, /gh/, /j/, /k/, /ng’/, na /th/; matamshi yasiyo sahihi ya maneno yanayotanguliwa na nazali /n/; uchopekaji wa sauti /u/, /w/ na /j/ katika maneno ya Kiswahili, udondoshaji wa sauti kama /h/, /a/, na /i/ katika maneno ya lugha hiyo, ubadilishanaji wa fonimu /r/ na /l/, na athari ya sauti /c/ ya Kinyarwanda katika otografia ya maneno ya Kiswahili. Makosa haya yanachochewa na athari za Kinyarwanda (L1) katika ujifunzaji wa Kiswahili (L2). Hivyo, utafiti wetu ulibainisha mikakati mbalimbali ya kutumiwa na walimu wa Kiswahili ili kukabili makosa ya kimatamshi na kiotografia yanayofanyika miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha tano. Mikakati hiyo ni pamoja na mbinu ya kuigiza tamthilia na mazoezi ya kimazungumzo, mrejesho wa moja kwa moja, utoaji wa kazi za kimaandishi kwa wanafunzi, na matumizi ya kamusi darasani. Aidha, utafiti huu ulipendekeza uundaji wa klabu za Kiswahili, utoaji wa zana za kidigiti katika ufundishaji wa Kiswahili, na kujumuisha somo la Kiswahili katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha tatu. Utekelezaji wa mapendekezo haya utasaidia kukuza umahiri wa wanafunzi katika matamshi na uandishi sahihi wa Kiswahili kama lugha ya pili. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Makosa, Matamshi, Otografia, Ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili en_US
dc.title Uchunguzi wa makosa ya kimatamshi na kiotografia yanayofanywa na wanafunzi wa kiswahili: Mfano wa shule teule za sekondari wilayani Nyarugenge, Rwanda en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account