University of Rwanda Digital Repository

Nafasi ya fasihi simulizi katika ukuzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza Kiswahili: mfano wa shule teule za sekondari wilayani Nyagatare

Show simple item record

dc.contributor.author Bisamaza, Emilien
dc.date.accessioned 2025-08-25T12:37:31Z
dc.date.available 2025-08-25T12:37:31Z
dc.date.issued 2022-06
dc.identifier.uri http://dr.ur.ac.rw/handle/123456789/2289
dc.description Master's Dissertation en_US
dc.description.abstract Tasnifu hii ni matokeo ya utafiti wenye anwani “Nafasi ya Fasihi Simulizi katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Stadi za Kusikiliza na Kuzungumza Kiswahili: Mfano wa Shule Teule za Sekondari Wilayani Nyagatare,” ambao ulikuwa na lengo kuu la kuchunguza nafasi ya fasihi simulizi katika kufundisha na kujifunza stadi za kusikiliza na kuzungumza. Malengo mahsusi yalikuwa kubainisha nafasi ya fasihi simulizi kufundishia na kujifunzia stadi za kusikiliza na kuzungumza, na kuunda mwongozo wa kutumia fasihi simulizi kufundishia na kujifunzia stadi hizo. Ukusanyaji wa data ulifanywa kwa ushuhudiaji, mahojiano na uchanganuzi wa matini. Walengwa wa utafiti huu walikuwa wanafunzi na walimu wa Kiswahili katika shule mbili za Wilaya ya Nyagatare. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Nadharia ya Utambuzi ndiyo iliyoongoza utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa fasihi simulizi ina nafasi muhimu katika ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza. Fasihi simulizi inawavutia wanafunzi, wakawa na motisha ya kujifunza bila uchovu. Hii inatokana na kuwa fasihi simulizi hutumia miktadha anuwai ya maisha ya kila siku na misamiati rahisi inayowawezesha wanafunzi kuelewa na kuzingatia usikilizaji na uzungumzaji. Kutokana na haya, mwongozo wa kutumia fasihi simulizi kufundishia stadi za kusikiliza na kuzungumza uliundwa, ili kuwaongoza walimu kufundisha stadi hizi. Mwongozo huu, unawasilisha mambo ya kuzingatia kwa kila hatua ya somo, kuanzia mandalizi ya somo, utoaji wa somo na tathmini. Mapendekezo mbalimbali yametolewa kwa wadau mbalimbali, ili kufanikisha uungaji mkono na kutiliwa maanani kwa ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza kama stadi za msingi. en_US
dc.language.iso sw en_US
dc.subject Kiswahili en_US
dc.subject Kusikiliza na Kuzungumza Kiswahili en_US
dc.title Nafasi ya fasihi simulizi katika ukuzaji wa stadi za kusikiliza na kuzungumza Kiswahili: mfano wa shule teule za sekondari wilayani Nyagatare en_US
dc.type Dissertation en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Repository


Browse

My Account